31 March 2011

Mtoto wa Lowassa mbaroni kwa kumgonga trafiki

Na Masau Bwire

MTOTO wa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, Bw. Bernard Lowassa (30), anashikiliwa na Jeshi la Polisi Kituo cha Oysterbay, Kinondoni, Dar es Salaam kwa tuhuma za
kumgonga kwa makusudi askari wa Kikosi cha Usalama barabarani E 9320 Koplo Cyprian akiwa katika kutekeleza majukumu ya kazi.

Watu walioshuhudua tukio hilo waliaalaani na kuhoji sababu za mtoto huyo kufanya hivyo, wengine wakienda mbali zaidi wakidai pengine alifanya hivyo kwa kujiona hawezi kubanwa na sheria kwa kuwa ni mtoto
wa kigogo.

Tuko hilo lilitokea juzi saa 1 jioni eneo la Namanga, Oysterbay  katika eneo la taa za kuongoza magari.

Akiendesha gari lenye namba za usajili T 573 BQV, Corona Primio, kutoka Msasani kwenda Morocco, alikaidi utaratibu wa trafiki huyo wa kuruhusu magari kupita kwa awamu kwa kulazimisha kupita kabla hajaruhusiwa.

Koplo Cyprian pengine kwa lengo la kuepusha magari kugongana na kutaka kuchukua hatua ukaidi wa Bernard, alilazimika kumzuia asipite lakini, bila kujali wala woga, aliendesha gari lake na kumgonga katika mguu na kumsukuma.

Mshuhuda walioshuhudia tukio hilo walisema askari huyo aling'ang'ania gari hilo hadi madereva wengine walipomuokoa kwa kulizuia gari la kijana huyo baada ya kusimama mbele ya gari lake.

Baada ya madereva wengine ambao nao walikuwa wakisubiri kuruhusiwa kupita katika taa hizo kukerwa na kitendo alichokifanya Bernard kumugonga kwa makusudi.

Watu wakiwa na hasira nusura wamshushie kipigo mtoto huyo lakini, askari huyo liwasihi wasifanye hivyo bali waiache sheria ichukue mkondo wake.

Madereva hao walitii kauli ya askari huyo aliyekuwa akichechemea na kulia kwa uchungu kutokana na maumivu makali kutoka katika mguu

Polisi wa kituo hicho walifika katika eneo hilo na kumchukua mzobemzobe mtoto huyo hadi Kituo cha Polisi Oysterbay, na habari zaidi zinasema baadaye aliachiwa kwa dhamana kwa sharti la kutakiwa kuripoti kituoni leo.

Kamanda wa Jeshi la polisi, Mkoa wa Kipolisi Kinondoni Bw. Charles Kenyela alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba koplo Cyprian alipelekwa Hospitali ya Mwananyamala kwa matibabu.

Kamanda Kenyela alionesha kusikitishwa na kitendo hicho cha mtu kudhani kuwa yuko juu ya sheria.

"Nimesikitishwa na kitendo hicho, mtu anaamua kutokufuata sheria za
barabarani na kudharau kazi ya askari wakati wa kutekeleza majukumu yao.

"Kijana huyo amekamatwa na anahojiwa na polisi, tuiachie sheria ichukue mkondo wake na kuamua cha kufanya kuhusu kitendo hicho cha uvunjifu wa sheria kilichofanywa na kijana huyo wa Lowassa," alisema Kamanda Kenyela.

Askari wa vyeo vya chini wameonesha wasiwasi kuhusu hatua za kisheria zitakazochukuliwa dhidi ya mtoto huyo wa kigogo wakidai, kumekuwa na kawaida ya vigogo kulindana na kupoteza haki ya mtu
wa hali ya chini.

Mmoja ya askari ambaye hakutaka jina lake kutajwa gazetini alisema kwamba ana uhakika kuwa mtoto huyo atalindwa, hatafanywa chochote, zaidi kulazimishwa askari huyo kumsamehe.

22 comments:

  1. sioni km sheria itachukua mkondo wake, watu wangechukua sheria mkononi ndo adabu kwaa watu km hao.
    Askari wetu mjue sasa hao vigogo mnaojikomba kwao na kuminya haki za raia wa chini si wenzenu teteeni wananchi ndugu zenu.
    pole trafiki lakn sheria haitachukua mkondo wake ng'o.

    ReplyDelete
    Replies
    1. mbona hakukutengua kiuno kabisa? mmezidi matrafic. ingekuwa amri yangu hicho kitengo ningekifunga.

      Delete
  2. Askari jeshi la polisi mnadharauliwa na watoto wa vigogo kwani mmeacha majukumu yenu ya kuwalinda raia na mali zao na kuwa vibaraka wa mafisadi hao! Watoto wao wanajua hilo ndio maana wanawafanyia kama walivyomfanyia huyo askari wa usalama barabarani. We trafiki nenda kwa Lowassa akupe milioni moja kesi iishe!

    By the way, ile ishu ya askari kutaka kumbambikia mtoto wa Mengi madawa ya kulevya imeishia wapi? Ni swali tu kwa IGP na kamati aliyoiunda!

    ReplyDelete
  3. We mtoa maoni hapo juu kwani heshima ya jeshi la polisi na thamani ya askari wa jeshi hilo ni milioni moja tu? Acheni kudhalilisha jeshi letu, asipomshitaki mimi nitafungua mashtaka kama raia mwema.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Police walikuwa zamani. sasa hivi ni wafanyabiashara. wacha washikishwe adabu. na hata mimi akinikalia vibaya namtengua kiuno. nini mguu? wabambika kesi wao majambazi wao. tutaponea wapi? Hongera uliyemgonga.

      Delete
  4. Sheria ni msumeno wacheni kulaumu au kuhukumu kwa fikra zenu kutaka mahakama ihukumu mutakavyo nyinyi, huyo atafikishwa mahakamani na atapewa adhabu kulingana na kosa lake lakini...!! Adhabu nyingi za barabarani ni faini hakuna kufungwa,ukiwa hohehae labda utafungwa si zaidi ya miaka 5 tena ukiua. kitendo hiki kinabidi kilaaniwe kwa nguvu zote na vyombo vya habari vyote,unafikia kumgonga ukizingatia Askari wetu wanafanya kazi ktk mazingira magumu,magari mengi jua lao mvua yao, kipato kidogo,kazi ngumu na wanafanya kwa moyo wao wote leo unamdhalilisha hii ni mbaya sana

    ReplyDelete
  5. Napendanda kutoa pole kwa askari wetu wa trafic kwa maumivu pamoja na kudhalilishwa na huyo mtoto wa mafisadi.Ninacho omba sheria ichukue mkondo wake kwa huyu kijana kama ambavyo ingechukua kwa raia mwingine yule. Hii ni makusudi alifanya na wala si bahati mbaya, na makusudi haya yamekuwa yakifanywa na watoto wengi wa vigogo kwa kudhalilisha dola kama alivyo fanyiwa cyprian. Serikali ni mali ya watanzania na wala si mali ya lowasa kama anavyodhani huyo mpumbavu. Pole cyprian usikate tamaa tuko pamoja tutahakikisha haki imetendeka, macho ya watanzania yameliona hili. Nguvu ya mnyonge ni umoja! na nguvu ya umma ni nguvu ya Mungu..............

    ReplyDelete
  6. Kwanza kabisa nakupa pole sana Ndugu yangu Cyprian. Ni wazi kazi zenu zinataka uvumilivu sana. Jua lenu, mvua yenu, matusi yenu, n.k.
    Jambo ambalo naomba sasa ulifahamu ni kwamba binadamu wote wenye utu wanayajua masumbufu yenu na wanawahurumia. Nadhani umeona kwamba kitendo hicho cha kijana huyo mpumbavu alichokifanya kwako kiliwaudhi watu wote wenye nia njema na kutoa msaada kwako mara moja. Shukurani nyingi sana kwa huruma yako, kwa kweli angepigwa sana. Pesa na umaarufu wa baba yake visimfanye kwamba na yeye sasa ni wazizi mkuu aliyejiuzuru kwa tuhuma ya ufisadi. Ugua pole ndugu yangu.

    ReplyDelete
  7. Huyu askari atapewa hela ya matibabu na vitisho basi yamekwisha. Askri anavyopenda hela. Milioni moja inatosha atawekwa kwenye line.

    ReplyDelete
  8. Hapa patamu kweli. Askari wa Jeshi la Polisi avunjwe vunjwe kabisa na hako katoto ili wenzake wajifunze kwani hawa si ndio hao hao waliua raia kule Arusha wakati wa maandamano. Kisa walipewa amri na wakubwa. Sasa mkuki kwa nguruwe mtamu je kwa binadamu.......!!
    Askari wamezoea kujikomba kwa viongozi walioko madarakani na kusahau walalahoi wenzao. Mwenye nacho anacho tu. Hafanywi lolote huyu mtoto wa kigogo mmesahau Andrew Chenge aliua watu wawili kwa mpigo? Si yuko tu huru anajichana atakavyo. Sembuse huyu ambaye hajaua amejeruhi tu mguu. Askari wanapenda sana chochote huyu akipewa chochote hakuna kesi hapa.
    Jamani ndugu zangu Maaskari mjifunze kutokana na makosa yanayofanyika.

    ReplyDelete
  9. Ndugu yangu askari ukitaka mambo yaende safi chukua chako mapema ukafie mbali lakini ukitaka haki itendeke utakula wa chuya my friend!!

    ReplyDelete
  10. Jamani wananchi muliokuwepo mumekosea, mungemshushia kipigo japo kidogo cha kumshikisha adabu ili na wengine wapate funzo kwamba hawako juu ya sheria.

    Masikini Askari Cyprian pole sana kauguze mguu wako wakati mwenzako anakula kuku kwa mrija, si unaona hata ndani hakuwekwa. Ingekuwa raia wa kawaida angekiona cha mtema kuni..

    Sasa kama unasubiri kesi utaendelea kusubiri sanaaaaaaaaaa.

    ReplyDelete
  11. huyo askiali anakihelele! angeacha wananchi wamchome moto ndiyo ajuwe kwamba askari wanawenyewe!!

    ReplyDelete
  12. Wasije wakageuza hiyo ikawa kesi ya ajali.Hii ni kesi ya mauaji (Attempt to kill by deadly weapon).Sijui ni kwa nini amepewa mzamana kirahisi namna hiyo.Huyo kijana antakiwa apewe adhabu ambayo itakuwa fundisho.

    ReplyDelete
  13. Huyo mtoto wa FISADI alitakiwa ashushsiwe kisago palepale, ningekuwepo mbona ningemzomea, analeta ufisadi wa babake anayetaka kujisafishia njia amtawale nani hapa 2015. Jeuri ya fedha za babake hizo na tuone kama sheria itachukua mkondo wake, jeuri jeuri nchi ya kwake peke yake? huyo kwanza anatakiwa aripoti polisi asubuhi mchana na jioni ndio dawa yeke na wananchi tunasema ASKARI WETU APONE TENA WAMUHUDUMIE APONE HATUTAKAA KIMYA SHERIA ICHUKUWE MKONDO WAKE. Askari alikuwa kazini leo kafisadi mtoto kanajitia jeuri na hilo gari lishikiliwe ili huyo babake anayejiita mheshimiwa sana anataka kujisafishia njia aende polisi kuwaleta za kuleta ili amkomboe mtoto wake sheria hapo itumike.

    ReplyDelete
    Replies
    1. FISADI WEWE NA BABA YAKO NA MAMA YAKO. ALIKUFISADI NINI?

      Delete
  14. Kamanda Mpinga na Kamanda Vitus mnaona vijana wenu wanavyonyanyasika na watoto jeuri wa vigogo. Huyo mtoto Bernard jeuri na jeuri ni ya babake marichmond hao kibao, sheria ichukuwe mkondo wake huyo kijana wenu alikuwa kazini leo mwendesha gari sheria haijui ya kuendesha gari kwa ujeuri wa familia yenye pesa. Wananchi tutapenda tujulishwe kesi hii imefika wapi, hatukufurahishwa kuumizwa kwa trafiki huyo, wakati huu watanzania hatutakiwi tukae kimya kwa hawa wasiofuata sheria za barabarani.

    ReplyDelete
  15. Pole sana ndugu trafiki kwa madhila yaliyokukuta.Haya ndiyo madhara ya kuwalea mafisadi ndiyo maana watoto na jamaa za hao mafisadi wanajiona wapo juu ya sheria.Haya hima wananchi tusiwaache mafisadi wafanye wanavyotaka.

    ReplyDelete
  16. Wachangiaji wengi hapa inaonyesha hamna hoja bali ni kumshambulia Mh. Lowassa bila kujali kuwa ajali haona kinga haina Kikwete wala Lowassa, Mkulima wala waziri. Mimi namfahamu sana Benard Lowassa hana tabia chafu ya kuwagonga watu kama hiyo wala si mtoto wa Lowassa bali ni mdogo wa Lowassa. Pamoja na kutoka katika familia hiyo ya Lowassa Benard ni mtu wa kawaida sana kama walivyo watoto na ndugu wengine wa Lowassa. kwanza Lowassa mwenyewe amewalea watoto wake na kuwafundisha kujitegemea na kutambua kuwa kuwa cheo cha baba au mama yao si chao wala mali bali wanahitajika kufanya kazikwa bidii na kutafuta ya kwao. Hawa watoto ndivyo walivyo na familia hiyo iko hivyo.nenda monduli utajionea mwenyewe ni watu hao wanaishi maisha ya kawaida. Mimi naamini kuwa Bernad kama binadamu hawezi kufanya makusudi ya namna hii kwani nchini kuna sheria na yeye hayupo juu ya sheria. Hapa yawezekana huyu trafic alikuwa na matataizo pia kwani tunawajua matrafikiwwetu wa bongo walivyo ni idara inayonuka rushwa. Benard kama ni sheria ifuate mkondo wake lakini asihukumiwe kwa vile ni mtoto wa familia ya Lowassa hii ina maana kuwa watoto wa viongozi wasiendeshe magari kwa vile wakipata ajali basi ni kwa sababu yan ukubwa wa Baba zao. Watanzania tumepata wapi upungufu wa akili wa namna hii kejeli na dharau kwa lowassa kwa kumwita fisadi eti kwa sababu tu aliwajibika kisiasa kwa kujiuzuru wadhifa wake huu kabisa ni upungufu wa akili. Duniani hakuna kiongozi muungwana kama lowassa.Mtu nayekubali kuachia raha ya kodi za watanzania kwa ajili ya wengine yuko wapi hapa Tanzania zaidi ya Lowassa. Huyu mtu ni muungwana sana, mcha mungu asiyependa makuu, mweledi na mchapakazi ambaye kama bado angekuwa waziri mkuu leo Tanzania ingepiga hatua kubwa. Najua wapo watu kwa sababu zao binafsi hawampendi Lowassa. Lowassa ni binadamu kama ulivyo wewe, hakai mbinguni bali anakaa duniani, tena utamwona Monduli, Dar na sehemu nyingine Tanzania. Si lazimishi umpende Lowassa lakini hoja yangu ni kuwa awe fisadi kama kweli ameiba lakini asiitwe tu na kudhalilishwa kwa vile ni Lowassa. Kama kweli Lowassa angukuwa amehusika na Richmond nakuapia sasa angekuwa jela kwani ni adui wa wengi kisiasa na nyie mnaofuata mkumbo pia ni adui yenu bila sababu. Lakini Lowasa hakuhusika ndio maana leo yuko huu mitaani kama wewe. Ombi langu ni kuwa kitu kidogo kama ben kugonga mtu barabarani nayo ni habari ya Lowasa? Huu ni uandishi au ukihiyo!

    ReplyDelete
  17. kama vipi sheria ichukuwe mkondo wake hakuna kuoneana huruma kwani wote ni binadamu na hakuna aliye juu ya sheria.

    ReplyDelete
  18. Hamna mahakama tanzania,mahakama ni za kuwahukumu walalahoi tu,nchi haina sheria iliyo msumeno,na kama upo ni butu haukati. Mahakimu,majaji,makarani wao na mawakili ni wapenda pesa tu hao.hamna sheria,waache wapate raha ya mashaka duniani lakini kwa Mungu watakiona

    ReplyDelete
  19. @ Davie..
    Uhuru wa kuongea unaheshimiwa ila inafika mahali uache ukweli uchukue nafasi.Hivi unadhani ni mtanzania gani hamjui Lowassa(resigned)?kwa suala hili hatuhitaji utuelezee sana.we have facts and dont fool us with bluffs.maisha ya familia ya huyo bwana hayatuhusu.amefanya ajali mi nimeshuhudia unamtetea nini?huyo aliyejiuzulu tunamjua in and out...ukweli upo wazi acha ufahamike...hatuhitaji kama watanzania kuandikiwa full scapes za maelezo kumtetea mtu afterall kama ni mtu msafi kwanini asemwe.kwanini asipakaziwe Magufuli au mwingine???sheria ifuate mkondo wake...acha wafu wazikane...

    ReplyDelete